Mataifa matatu ya Afrika Magharibi
ambayo yalikuwa yakikabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola,
yamekamilisha wiki moja bila ya kuwa na mgonjwa yeyote wa ugonjwa huo
ulioanza mwaka 2014.
Mlipuko wa ugonjwa huo hatari umeuwa
watu 11,000 katika mataifa ya Guinea, Liberia pamoja na Sierra Leone,
kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
Matukio ya kesi mpya za wagonjwa wa
Ebola yameshuka mno mwaka huu, hata hivyo shirika la WHO limeonya
ugonjwa huo unaweza ukalipuka tena.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni