.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 8 Oktoba 2015

TUNAJITAHIDI KUTEKELEZA SERA NA MIPANGO YA MAENDELEO JUMUISHI - TANZANIA

Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akichangia majadiliano kuhusu ajenda ya Maendeleo ya Jamii katika Mkutano wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kamati Sita zinazounda Baraza hilo zimeanza mikutano yake ikiwa ni wiki moja tangu kukamilika kwa mikutano ya Kilele ya Viongozi wa Kuu wa Nchi na Serikali iliyofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

                                                                              Na Mwandishi Maalum, New York

Ikiwa ni Wiki moja kupita tangu Viongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa mbalimbali Dunia,

kuhitimisha ushiriki wao katika mikutano muhimu mikuu miwili, upitishwaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu na Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Nchi wanachama wameingia katika hatua nyingine ya mikutano ya Kamati Sita zinazounda Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Kamati zinazounda Baraza Kuu na ambazo zimeanza mikutano yake kuanzia jumanne na itakayo kwenda hadi mwezi desemba kwa baadhi ya Kamati , ni Kamati ya Kwanza ambayo baadhi ya majukumu yake ni pamoja na udhibiti wa matumizi holela ya silaha za aina mbalimbali zikiwamo silaha za nyukilia , kemikali, silaha ndogo , kubwa na nyepesi , upokonyaji wa silaha na masuala yahusuyo ulinzi na usalama

Mikutano ya Kamati ya pili nayo imeanza, kamati ya pili inahusika na masuala yote ya uchumi, ikifuatia na Kamati ya Tatu inayohusika na masuala ya maendeleo ya Jamii, Utamaduni na Haki za Binadamu. Imeanza pia mikutano ya Kamati ya Nne inayohusika na masuala ya kumaliza ukoloni, operesheni za ulinzi wa Amani na masuala ya mawasiliano ya Umma,

Kamati nyingine ambazo zinaunda Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ni Kamati ya Tano ambayo inahusika na masuala ya Bajeti na Utawala ikifuatia na Kamati ya Sita inayohusika na masuala ya, pamoja na mambo mengine, sheria za kimataifa, utawala wa sheria na mahakama za kimataifa.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu, inashiriki vema katika mikutano na mijadala yote ya Kamati hizi, ushiriki ambao pia unawahusisha wataalamu wa fani na kada mbalimbali kutoka Wizara na Idara za pande zote mbili za Muungano.

Akichangia majadiliano ya Kamati ya Tatu kuhusu ajenda ya Maendeleo ya Jamii,moja ya kati ya ajenda zitakazojadiliwa na Kamati hii, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi amesema, Tanzania imendelea na jukumu la kuhakikisha kwamba hakuna mtu wa rika lolote anayeachwa nyuma katika ajenda hiyo.

Akasema kuwa baadhi ya mikakati inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Muungano ni pamoja na kuhakikisha kwamba makundi yote ya jamii, yanapata fursa na haki ya kushiriki katika utoaji wa maamuzi wa mambo yanayowahusu.



Balozi Mwinyi, amefafanua kwa kutoa mifano kadhaa ya kisera na kiutendaji na jumuishi inayolenga katika kuwanufaisha na kuboresha maisha ya vijana, wazee, wanawake, watoto wa kike, na makundi mengine ya jamii kama vile watu wasiojiweza.
 

Akaeleza kuwa sera na mikakati hiyo inayolenga katika kumwondoa mtanzania katika umaskini ni pamoja na mipango ya uboreshaji na uendelezaji wa sekta mbalimbali ikiwamo ya kilimo inayojari watanzania wengi, uboreshaji wa sekta ya elimu na miundo mbinu yake kwa kuongeza bajeti, upatikanaji wa huduma za afya na kwa gharama nafuu hususani kwa wazee na watu wasojiweza.
 

Balozi Mwinyi ameeleza pia kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafanya kila iwezalo katika kuhakikisha kwamba kila mtoto wa kitanzania anapata fursa ya kupata elimu na si bora elimu lakini kwa kuhakikisha kwamba elimu anayopewa ni bora na yenye viwango vinavyo kubalika kitaifa na kimataifa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni