Wabunge nchini Kenya wamekasirishwa
mno na kitendo cha bunge kukatiwa umeme kwa siku tatu kutokana na
kushindwa kulipwa bili ya umeme yenye thamani ya dola 97,000.
Wabunge wa vyama vya upinzani
wameitupia lawama serikali, hata hivyo wabunge wa muungano wa Jubilee
unaotawala wameitetea serikali.
Wabunge hao pia wamesema hawajalipwa
posho zao na baadhi ya watumishi wa bunge hawajalipwa mishahara yao.
Mbunge Adan Keynan amesema umeme katika bunge la Kenya ulikatwa
Ijumaa hadi Jumatatu ya wiki hii.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni