Timu ya Chelsea imejisahaulisha
machungu yake ya Ligi Kuu ya Uingereza, na kusonga mbele kilaini
katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kupata ushindi
wa mabao 2-0 dhidi ya Porto.
Mbrazili Willian aliihakikishia
Chelsea kutinga katika hatua ya mtoano baada ya kufunga kwa shuti la
yadi 20 katika kipindi cha pili, baada ya Poro kujifunga bao la
kwanza katika kipindi cha kwanza.
Kipa Iker Sasillas akiokoa shuti la Diego Costa
Naye mshambuliaji Olivier Giroud
aliibeba Arsenal kutinga katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabigwa
Ulaya baada ya kupachika mabao matatu mwenyewe yaani hat-trick dhidi
ya Olympiakos.
Giroud alianza kupachika bao la
kwanza katika dakika ya 29, na kisha kuongeza la pili dakika nne
baada ya kuanza kwa kipindi cha pili na kisha kupachika bao la tatu
kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 79, hata hivyo mchezaji huo
baadae aliumia mguu.
Kocha Arsene Wenger akifurahi ushindi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni