.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 8 Desemba 2015

CHINA KUPITIA JIMBO LA JIANGSU YATOWA MSAADA WA DAWA WENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 500

kom1 
Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Xie Yunliang akitoa maelezo wakati wa sherehe ya kukabidhi msaada wa dawa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500 zilizotolewa na Jimbo la Jiangsu kwa ajili ya Wananchi wa Zanzibar. Sherehe hiyo ilifanyika Bohari Kuu ya Madawa Maruhubi Mjini Zanzibar. na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
kom2
Baadhi ya Madaktari wa China na waalikwa wakifuatilia sherehe ya makabidhiano ya msaada wa dawa mbali mbali za binaadamu katika sherehe iliyofanyika Bohari Kuu ya Madawa Maruhubi.
kom3
Kamishna wa Afya na Uzazi wa Mpango ambae pia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jimbo la Jiangsu Hong Hao akizungumza wakati wa makabidhiano ya dawa zenye thamani ya shilingi milioni 500 (kulia) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabiti Kombo.
kom4
Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Xie Yunliang na Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo wakitia saini makabidhiano ya dawa hizo zilizotolewa na Jimbo la Jiangsu.
kom5
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na Balozi mdogo wa China wakibadilishana hati za makabidhiano ya msaada wa dawa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500 katika sherehe zilizofanyika Bohari Kuu ya Madawa Maruhubi.
kom6
Balozi mdogo wa China akimkabidhi Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo sehemu ya Dawa zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia Jimbo la Jiangsu (kati) Naibu Mkurugenzi Mkuu ambae pia ni Kamishna wa Afya na Uzazi wa Mpango wa Jimbo hilo Hong Hao. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.​

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni