.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 10 Desemba 2015

HOSPITALI ZA APOLLO IPO MSTARI WA MBELE KUOKOA MAISHA YA WAHANGA WA MAFURIKO MJINI CHENNAI


Chennai ni jiji la tano kwa ukubwa nchini India, jiji hilo limepigwa na janga
kubwa la mafuriko ambayo hayajawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 100
iliyopita, mafuriko hayo yameliacha jiji hilo likiwa hoi na taabani.

Mafuriko hayo ya kihistoria yalisababisha jiji hilo kukosa huduma muhimu
 kama umeme, maji safi, chakula, usafiri na mahitaji mengine ya msingi.
Idadi ya wagonjwa wengi wameripotiwa kufariki baada ya maji ya mvua
kubwa kuharibu majenereta na mfumo mzima wa umeme kwenye hospitali
mbalimbali mjini humo.

Kufuatia  mafuriko hayo makubwa jiji Chennai, hospitali za Apollo zilizopo
Chennai zimeripotiwa kuwa zinaendelea kufanya kazi vizuri na kuwa mstari
 wa mbele kutoa huduma kwa waathirika wote wa hayo mafuriko. 

Wakati
hospitali nyingi Chennai zikiwa zinasumbuka na tatizo la umeme;
hospitali za Apollo zina endelea kutoa huduma bora na kuzidi kutumia
timu yao ya wataalamu waliojikita katika kuokoa maisha ya watu wengi. 

Preetha  Reddy, Makamu Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo, alisema wametenga timu  30 zenye wataalamu wa afya kama 300 katika kukabiliana na wahanga hao  wa mafuriko.

Kwa mujibu wa  Sathyabhama, mkurugenzi wa huduma za afya na ubora wa kanda ya  kaskazini katika hospitali za Apollo; hospitali ya Apollo imepokea
wagonjwa wengi kutoka hospitali nyingine nyingi mbalimbali zilizokumbwa na ukatikaji wa umeme kutokana na mafuriko.


Mwendelezo wa huduma kutoka hospitali za Apollo katika sehemu mbalimbali jijini  umesababisha wagonjwa kutohamishiwia hospitali nyingine, licha ya
kupokea zaidi ya wagonjwa 50 ambao wengine ni wageni nchini India kutoka
 hospitali nyingine zilizoathirika na janga hilo, alisema.

Wagonjwa ambao ni wageni nchini India kutoka nchi zaidi ya 20 waliokuwepo
hospitali za Apollo walipewa kadi ya mawasialiano ya ISD na huduma ya
mtandao ili waweze kuwasialiana na familia zao, alisema Dk. Srinidhi
Chidambaram makamu wa raisi wa idara ya wagonjwa kutoka mataifa
mbalimbali. Ndugu Ahmed Noumani kutokea Oman amedhibitisha kuwa ameona  ubinadamu wa ukweli kutoka hospitali za Apollo, alijiskia yupo salama na  mwenye ulinzi mzuri na pia kuwezeshwa kuwasiliana na familia yake muda  wote iliyopo nchi ya Oman.

Ongezeko kubwa la kiwango cha maji kwenye mabwawa ilipelekea mto Adyar kufurika  na kuleta majanga jijini na vijijini. Alisema umeme ulikatika kwa muda  wa masaa 57 katika jengo moja na masaa 69 jengo lingine lakini
waliendelea kufanya kazi kwa kutumia jenereta. Kwa ajili ya usalama,
umeme ulikatwa kwa siku kadhaa jijini Chennai na maeneo ya jirani yake.

Tunatoa
 kipaumbele katika huduma kwa wagonjwa. Ni yale matibabu ya dharura tu
na matumizi ya vifaa vya uokoaji ndivyo tulivyoshungulika navyo.
Kipaumbele kilikuwepo zaidi katika maeneo yaliyoathirika sana,” alisema Bi. Sathyabhama

Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, ukatikaji wa umeme ulifanyika kuanzia Ijumaa wiki iliyopita kwa sababu za kiusalama.

Kufuatia
 mvua kali zinazoambatana na upepo nchini India katika mji wa Tamil
Nadu, hospitali za Apollo zimetoa huduma bure za afya na kuweka vituo na
 kambi za matibabu kwa wahanga wote jijini Chennai.

Kambi iliwekwa katika ofisi ya baraza kuanzia saa tatu asubuhi. Timu ya
madkatari 20 inayojumuisha wataalamu wa magonjwa ya tumbo
(gastroenterologists), madaktari wa kawaida, wataalamu wa magonjwa ya
watoto (paediatricians),wataalamu wa magonjwa ya wanawake
(gynaecologists), wataalamu magonjwa ya shingo na kichwa (ENT
specialists),wataalamu wa uti wa mgongo na misuli (orthopaedicians), na
wataalamu wa magonjwa ya mapafu (pulmonologists) wakiwa na manesi 20 na
matabibu wengine kutoka Hospitali za Apollo waliwekwa kwenye hizo kambi.

Hospitali  za Apollo zimetoa mchango mkubwa sana katika kuokoa maisha ya wananchi  wengi wa India katika kipindi hiki cha mvua za mafuriko jijini Chennai.

Magwiji hao wanaongoza kwa huduma bora za afya ulimwenguni wameonyesha  mfano wa kuigwa wa namna vituo vya afya vinatakiwa kuwa bora na msaada  katika kuokoa maisha hasa pale majanga yanapoteka.

Kuhusu Hospitali za Apollo 

Hospitali ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira
 yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. 

Tunajitolea  kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na utafiti kwa ajili ya  jamii ya kibinadamu".Katika miaka 30 tokea  kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata  kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la  Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini
india.

Katika  safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka  nchi 120.Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710.Imefanya  upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000  za mishipa myembamba.

Imefanya upasuaji wa wa viungo unapita kiasi cha  idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na  zaidi.Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india,  zikiwa na teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji
unaotumia mashine za kiroboti.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni