.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 8 Desemba 2015

JESHI LA ULINZI KENYA LAKANUSHA KUHUSIKA NA MAUAJI YA WATU MANDERA

Jeshi la Ulinzi Kenya (KDF) limekana kuhusika na matukio ya kutoweka kwa watu pamoja na mauaji yaliyofanyika Mandera, ambapo kaburi walilozikwa watu wengi limebainika siku ya Jumapili usiku.

Kaburi hilo lenye miili ya watu 12, akiwemo mwanamke mmoja aliyetoweka katika hoteli yake eneo la biashara la Arabia tangu Alhamisi, limeibua hofu ya kurejea kwa matukio ya mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola katika eneo hilo ambapo polisi na jeshi wanapambana na wapiganaji wa Al Shabaab.

Msemaji wa KDF Kanali David Obonyo, amesema Jeshi la Ulinzi Kenya halihusiki kwa lolote kuhusiana na kaburi la watu wengi lililobainika Mandera, wala halihusiki na kutoweka kwa watu ama mauaji ya watu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni