Kamanda wa Polisi wa kikosi cha usalama Barabarani nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mohammed Mpinga pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Fasta Fasta, Prasad Acharya wakizindua huduma mpya kwa abiria wa bodaboda inayopatikana kwa njia ya mtandao wa simu za mikononi ijulikanayo kwa jina la “Fasta Fasta Services”. Huduma hiyo umwezesha abiria kupata huduma ya usafiri huo kwa kufuatwa mahali alipo.
Na Mwandishi wetu.
KAMANDA wa Polisi wa kikosi cha usalama Barabarani nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mohammed Mpinga ametoa onyo kwa wamiliki na mawakala wa usafiri wa mabasi yaendayo mikoani kutoongeza nauli kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka na wakibainika watachukulia hatua za kisheria pamoja na kufungwa jela.
Kamanda Mpinga alisema hayo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya kwa abiria wa bodaboda kwa njia ya mtandao wa simu ya mkononi ijulikanayo kwa jina la “Fasta Fasta Services” ambayo umwezesha abiria kupata huduma ya usafiri huo kwa kufuatwa mahali alipo.
Alisema kuwa imekuwa tabia ya wamiliki na mawakala wa usafiri wa mabasi yaendayo mikoani kuongeza nauli kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa.

Alisema kuwa ili kuwabaini wanao kiuka sheria hiyo, wameweka askari kanzu vituo vyote vya mabasi yaendayo mikoani kwa lengo la kuwakamata wahusika.
“Tumejipanga nchi nzima kukomesha uhalifu huu, si kwa kituo cha mabasi cha Ubungo tu, bali nchi nzima, tumewapandikiza abiria ambao watakuwa na kazi ya kutoa taarifa za kuwakamata wahusika,” alisema Mpinga.
Alifafanua kuwa mwaka jana, wamiliki na mawakala watano walifungwa jela kwa kosa kama hilo na mwaka huu wamedhamilia kuona kila mmiliki wa mabasi na mawakala wao wa ukatishaji tiketi wanashughulikia suala hilo.
Kuhusiana na huduma ya usafiri wa bodaboda ya Fasta Fasta, Kamanda Mpinga alisema kuwa huduma hiyo inawarahisishia madereva wa bodaboda kuweza kuongeza kipato, kuondoa uhalifu na usalama wa mali zao.
Alisema kuwa huduma hiyo itamwezesha dereva na abiria kujuana na hata tatizo linapotokea, ni rahisi kujua nani wa kumkamata kwa ajili ya masuala mengine ya kisheria.
“Huduma ina mwezesha abiria kupata usafiri mahala popote alipo, anatakiwa kujiunga kupitia simu yake ya mkoni kwa ‘kudownload application’ na kuzijua bodaboda zote zilizomo katika huduma hiyo na kutuma ujumbe mahali ulipo na unataka kwenda wapi, dereva wa bodaboda atakujibu na atakuja kukuchukua mahali ulipo na hata nauli italipa kwa umbali wa kilometa,” alifafanua Mpinga.
Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Fasta Fasta, Prasad Acharya alisema kuwa kwa kuanza wameanza kuzindua huduma hiyo Dar es Salaam na baada ya mwezi Februari mwakani, watapanua wigo kwa kuzindua huduma hiyo mikoani. Acharya alisema kuwa mbali na pikipiki, huduma hiyo pia itazinduliwa kwa bajaji na taksi katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni