Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp
ameachwa akilalama kwa hasira baada goli la wazi la Alberto Moreno
alilolifunga kiufundi kukataliwa na refa kwa madai ya kuotea katika
mchezo wao na Newcastle United hapo jana.
Wakati Liverpool ikijaribu kuchomoa
bao 1 waliofungwa zikiwa zimebakia dakika 10 kabla ya mpira kuisha,
beki huyo wa kushoto alipanda mbele kushambulia na kupata pande
kutoka kwa James Milner ambapo aliudokoa mpira na kufunga goli hilo
lililokataliwa.
Hata hivyo goli hilo la mchezaji
huyo raia wa Hispania, ambalo lingeweza kuingia katika rekodi ya goli
la mwezi kwa mujibu wa Klopp, lilikataliwa na refa na baadae
Newcastle United ikaandika balo la pili na kufanya matokeo kuwa 2-0.
Mchezaji wa Newcastle United Wijnaldum akifunga bao la pili
Wachezaji wa Liverpool wakiwa hoi baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Newcastle United
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni