Nchi ya Rwanda itafanya kura ya
maoni wiki ijayo ya mabadiliko ya Katiba ili kumruhusu rais Paul
kagame kuongoza taifa hilo kwa muhula wa tatu mwaka 2017, na huenda
akabakia madarakani kwa miongo mingine miwili.
Marekani na Umoja wa Ulaya zimeonya
hatua hiyo ya Rwanda na kusema inakandamiza misingi ya Demokrasia
katika taifa hilo, hali iliyomfanya rais Kagame kuyakosoa mataifa
yanayoingilia mambo ya ndani ya nchi yake.
Baraza la Seneti la Rwanda mwezi
uliopita lilipitisha mabadiliko ya Katiba kutoka vipindi viwili vya
maiaka saba vya urais na kufanya kuwa vipindi viwili vya miaka mitano
na kuagiza mihula miwili ya urais, isipokuwa kwa Rais Kagame ambaye
ameongezewa tena muhula mwingine 2017.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni