Mwenyekiti wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier Murcia akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Mseru leo wakati wa mkutano na viongozi wa jumuiya hiyo na wataalamu wa hospitali hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario wa MNH.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha akiwa katika mkutano huo uliofanyika leo kabla ya kukabidhiwa kwa vifaa vinavyotumika kuwasaidia wagonjwa wakati wa kupatiwa matibabu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier Murcia akiwa katika picha ya pamoja na wauguzi wa hospitali hiyo baada ya kukabidhiwa msaada huo leo.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Bi. Agness Mtawa akipokea msaada wa vitanda na vifaa vingine leo kwenye hospitali hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier Murcia akimkabidhi Sister Mtawa vifaa hivyo na kulia ni Mkurugenzi wa jumuiya hiyo, Thierry Murcia.
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vifaa mbalimbali vitakavyotumika kuwahudumia wagonjwa katika hospitali hiyo.
Msaada wa vitanda kumi utatumika katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na wodi nyingine. Msaada huo umetolewa na Jumuiya ya Australia na Tanzania.
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vifaa mbalimbali vitakavyotumika kuwahudumia wagonjwa katika hospitali hiyo.
Msaada wa vitanda kumi utatumika katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na wodi nyingine. Msaada huo umetolewa na Jumuiya ya Australia na Tanzania.
Vifaa vingine vilivyotolewa ni pamoja na Stretcher’ nne zitakazotumika kusafirishia wagonjwa ambao hawawezi kukaa, kifaa cha kufanyia mazoezi kwa wagonjwa na baiskeli ya magurudumu matatu.
Akipokea msaada huo Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika hiyo Agness Mtawa ameishukuru Jumuiya hiyo na kutoa rai kwa wadau wengine kuendelea kutoa msaada katika hospitali hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni