Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama amelitaka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuhakikisha linakabidhi daraja la Kigamboni ifikapo Januari, 2016.
Pia ametoa fursa kwa shirika hilo na mengine nchini kama yataweza kuja na mradi wa ujenzi wa daraja kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar.
Hayo alibainisha jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa daraja hilo, ambalo linatarajiwa kukamilika mwakani.
Alisema ujenzi wa daraja hilo, umegharimu kiasi cha Dola za Marekani 143.5, ambapo serikali imetoa asilimia 40, huku NSSF ikitoa asilimia 60 ya fedha zote.
“Tunaliomba shirika hili, lihakikishe linaheshimu nha kuzingatia muda uliotoa katika kukabidhi daraja hilo mwakani licha ya kujitokeza ujenzi mwingine wa barabara ya Kilomita moja,”alisema.
Alisema shirika hilo linapaswa kulikabidhi daraja ifikapo Januari 30 au kabla ya muda huo, kwani ukamilifu wake utapunguza adha ya foleni na kukuza sekta ya uchumi inayotarajiwa kukuwa kwa kasi.
Katika hatua nyingine, Mhagama alisema endapo mradi ukiwa katika ubora na viwango vinavyotakiwa utadumu kwa muda mrefu na kuisaidia Seriali katika kukuza uchumi.
Alisema shirika hilo linapaswa kulikabidhi daraja ifikapo Januari 30 au kabla ya muda huo, kwani ukamilifu wake utapunguza adha ya foleni na kukuza sekta ya uchumi inayotarajiwa kukuwa kwa kasi.
Katika hatua nyingine, Mhagama alisema endapo mradi ukiwa katika ubora na viwango vinavyotakiwa utadumu kwa muda mrefu na kuisaidia Seriali katika kukuza uchumi.
“Miradi ya namna itasaisdia kukuza uchumi wa ndani na nje ya nchi, pia inatufundisha kujifunza ili kujua kwamba tunaweza kuhimili miradi mingine mikubwa zaidi ya huu,”alisema.
Kuhusu daraja la kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar, alisema uwezekano wa kujengwa upo endapo mashirika yakijitokeza na mradi huo. “Kila kitu kinawezekana, hivyo kama Shirika litajitokeza serikali ipo tayari kwa kila kitu kuunga mkono mkakati watakao kuja nao,”alisema.
Naye Mkurungenzi wa NNSF, Dk.Ramadhan Dau alisema ujenzi wa daraja hilo umekuwa wa kasi licha ya matatizo yaliyojitokeza, hivyo Watanzania watarajie Januari mwakani kulitumia.
“Bado kuna sehemu nyingine ambazo tutamalizia ila hadi Januari litakuwa limekamilika kwa asilimia 100, hivyo tunaipongeza serikali kwa ushirikiano uliotuonyesha,”alisema.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni