.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 24 Desemba 2015

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAWAZIRI KUJAZA NAFASI ZILIZOKUWA WAZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa  Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la  Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano ya utawala wake.

                                                                                  Uteuzi huo ni kama ifuatavyo:-

1. Profesa Jumanne Maghembe – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

2. Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).

3. Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

4. Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)

5. Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

6. Prof. Makame Mbarawa – Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano

Katika hatua nyingine Rais wa nJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na  kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

23 Desemba 2015

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni