Serikali ya Somalia imepiga marufuku
sherehe za Krismasi na mwaka mpya katika Jiji la Mogadishu, kutokana
na sherehe hizo kutoendana utamaduni wa dini ya Kiislam na zinaweza
kuhatarisha usalama.
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Masuala
ya Dini Sheikh Mohamed Khayrow ametangaza uamuzi huo wa kupiga
marufuku sherehe hizo za mwisho wa mwaka Jijini Mogadishu akiwa na
Makamu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Dini Sheikh Nur Barud Gurhan.
Sheikh Nur Barud Gurhan, amesema
mikusanyiko yoyote haipaswi kuwepo Jijini Mogadishu, na kuongeza kuwa
sherehe za Krismasi zinaweza kuwahamasisha wapiganaji wa
al-Shabaab kufanya mashambulizi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni