Shirika la Ujasusi la Marekani FBI
limesema wanandoa waliofanya tukio la shambulizi la San Bernardino na
kuuwa watu 14 walingizwa katika itikadi kali kabla ya kuanza
mahusiano yao.
Bw. James Comey amesema Tashfeen
Malik na mumewe Syed Farook walizungumzia masuala ya Jihad katika
mazungumzo yao kwenye mtandao wa kutafuta wenza mwaka 2013.
Shirika la FBI linaamini wanandoa
hao walifanya tukio hilo kutokana na kuvutiwa na matukio ya makundi
ya kigaidi, hata hivyo uchunguzi unaendelea.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni