.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 9 Desemba 2015

WAANDISHI WA HABARI NA SIKU YA UHURU

ZANZIBAR, KLABU YA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR (ZPC) LEO INATARAJIA KUUNGANA NA WATANZANIA WENGINE KUADHIMISHA SIKU YA UHURU WA TANZANIA BARA KWA KUFANYA USAFI KATIKA HOSPITALI YA WAGONJWA WA AKILI ZANZIBAR ILIYOPO KIDONGO CHEKUNDU, WILAYA YA MJINI, MKOA WA MJINI MAGHARIBI, UNGUJA.

KWA MUJIBU WA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA KATIBU MTENDAJI WA KLABU HIYO FAKI HAJI MJAKA ALISEMA KUFANYA HIVYO PIA NI KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JOHN POMBE MAGUFULI ALILOLITOA SIKU CHACHE BAADA YA KUINGIA MADARAKANI.

KWA MUJIBU WA AGIZO LA DK. MAGUFULI ALIAHIRISHA MAADHIMISHO YA MWAKA HUU YA SHEREHE HIZO KWA GWARIDE NA BADALA YAKE AMEWATAKA WATANZANIA WAITUMIE SIKU HIYO KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA IKIWA NI SEHEMU YA KUIDUMISHA DHANA YA UHURU NA KAZI.

MJAKA AMESEMA UAMUZI WA KLABU YAKE KUADHIMISHA SIKU HIYO KATIKA HOSPITALI HIYO MBALI YA KUWEKA MAZINGIRA YA ENEO HILO KATIKA HALI YA USAFI, PIA UMELENGA KATIKA KUIHAMASISHA JAMII KUJITOLEA NA KUFANYA KAZI KATIKA MAENEO YA KIJAMII ILI KUONDOA DHANA YA UNYANYAPAA KWA MAKUNDI HAYO.

AMESEMA WAGONJWA WA AKILI NI MIONGONI MWA KUNDI LINALOHITAJI UANGALIZI WA KARIBU WA WANAJAMII MBALI YA MADAKTARI WANAOWAHUDUMIA.

AIDHA AMEUSHUKURU UONGOZI WA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR NA HOSPITALI YA KIDONGO CHEKUNDU KWA JUHUDI WANAZOCHUKUA KATIKA KUIWEKA HOSPITALI HIYO KATIKA MAZINGIRA MAZURI NA KUWATAKA WADAU WA HABARI NA WANACHAMA WA KLABU HIYO KUJITOKEZA KWA WINGI KUIADHIMISHA SIKU HIYO.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni