Kocha Manuel Pellegrini amesema
mshambuliaji wake Sergio Aguero atarejea katika kiwango chake na
kusaidia Manchester City kuwania taji la Ligi Kuu ya Uingereza.
Mshambuliaji huyo raia wa Argentina,
27, alifunga goli la ushindi dakika za mwisho katika matokeo ya
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Watford, na kuwa nyuma kwa pointi tatu
dhidi ya kinara wa ligi timu ya Arsenal.
Mchezo huo ulikuwa watatu kwa sergio
Aguero kucheza baada ya kuwa nje ya uwanja mwezi mmoja kwa jeraha la
goti, ambalo alilipata baada tu ya kupona misuli ya mguu.
Sergio Aguero akiwa ameruka juu kufunga mpira wa kichwa na kuibeba Man City
Nayo Arsenal imekwea kileleni mwa
ligi kwa pinti mbili juu dhidi ya Leicester katika Ligi Kuu ya
Uingereza baada ya kuifunga Newcastle bao 1-0.
Arsenal ambayo ilionekana kutokuwa
na uhakika wa kuondoka na ushindi katika dimba la nyumbani la
Emirates Stadium, ilipata bao lake pekee kupitia beki Laurent
Koscielny katika dakika ya 72.
Laurent
Koscielny akifunga bao pekee lililoipa ushindi Arsenal
Matokeo mengine ya Ligi hiyo ni ni:-
West Ham 2 - 0 Liverpool, Leicester 0 - 0 Bournemouth, Man Utd 2 - 1
Swansea, Norwich 1 - 0 Southampton, Sunderland 3 - 1 Aston Villa
pamoja na West Brom 2 - 1 Stoke.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni