.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 4 Januari 2016

MATOKEO YA AWALI YA URAIS KATIKA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI TOUADARE AONGOZA

Matokeo ya awali ya urais katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yanaonyesha waziri mkuu wa zamani Faustin Archange Touadera anaongoza katika hali ambayo haikutarajiwa.

Wagombea 30 waliwania urais katika uchaguzi huo ambao huenda ukawa na marudio baina ya wagombea wawili wa juu Januari 31.

Bw. Touadera ambaye alikuwa waziri mkuu wa serikali ya rais aliyeng'olewa madarakani 2013 na waasi wa Seleka Bw. Francois Bozize.

Upigaji kura ulifanyika Desemba 30, huku vikosi vya Umoja wa Mataifa vikilinda vituo vya kupigia kura.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni