Miili ya watu 34
imesombwa na maji katika pwani ya Uturuki ikiwa ni janga la hivi
karibuni lililowakumba wahamiaji na wakimbizi wanaokatiza bahari ya
Ugiriki.
Boti ya wahamiaji hao
inasadikiwa kuwa kuzama wakati ikikatiza kisiwa cha lesbos.
Miili yao imekutwa
kwenye fukwe za Ayvalik na Dikili umbali wa kilomita 50 kutoka sehemu
nyingine, wengi ya waliofariki ni watoto.
Zaidi ya wahamiaji
milioni moja wamekatiza bahari ya Mediterranean mwaka 2015 na wengi
wao wameenda Uturuki na Ugiriki.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni