Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,Mh.Mwigulu Lameck Nchemba akisikiliza kero za wadau wa machinjio ya Vingunguti usiku huu wa January 1/01/2016.
Mwigulu Nchemba akishuhudia Ng’ombe aliyetayari kwa taratibu za kuchinjwa kwaajili ya kitoweo.Katika hatua ya kushitukiza,Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba amefanya ukaguzi wa Machinjio ya Vingunguti usiku huu.
Mh.Mwigulu Nchemba amefika kwenye Machinjio hayo usiku huu ilikushuhudia Mifugo ikiandaliwa kwaajili ya kitoweo cha wananchi.Uchinjaji wa Ng’ombe na Mbuzi katika machinjio haya hufanyika nyakati za Usiku kuanzia saa 4 hadi 10 alfajiri.
Mbali na kusikiliza kero na maoni ya wananchi kuhusu uendeshwaji wa Machinjio hayo,Mwigulu Nchemba ameshuhudia utafunwaji wa kodi ya serikali inayokusanywa kwenye mnada wa pugu.
Utafunwaji huo unatokana na uandikaji wa kibali cha mifugo michache kuja Machinjioni ili hali mifugo Zaidi huingizwa machinjioni bila kibali.Matharani hii leo Mh.Waziri ameshuhudia Ng’ombe waliotoka mnada wa pugu ambao wameshalipiwa kodi wakiwa 1450 lakini kibali chake kimeandikwa Ng’ombe 300 tu.Inamana kuna ng’ombe 1150 wamelipiwa ushuru lakini machinjioni kimeletwa kibali cha ng’ombe 300 wakati kwa kuwahesabu ng’ombe hao wanazidi 1000.
Kutokana na hali hiyo,Mh.Waziri ameagiza wahusika wote kufika kesho kwenye mkutano wa asubuhi kwaajili ya hatua stahiki kuchukuliwa,Mwigulu amesisitiza kuwa kwa mtu yeyote mwenye dhamana na kusimamia sekta ya kilimo,Mifugo na Uvuvi afanya kwa mujibu wa sharia,vinginevyo hakutakuwa na huruma kwa wanaohujumu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni