Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 kwa Wachezaji wa Ndani, mchezaji wa Taifa Stars na Klabu ya TP Mazembe ya DRC Congo, Mbwana Samatta.
BAADA ya kushinda Tuzo ya Afrika kama Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 kwa Wachezaji wa Ndani, mchezaji wa Taifa Stars na Klabu ya TP Mazembe ya DRC Congo, Mbwana Samatta anatarajiwa kupongezwa na kuagwa rasmi na mashabiki wake leo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Akizungumza na Uwazi, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa mapema kabla ya saa kumi na mbili jioni kutakuwa na matembezi sambamba na Samatta maeneo ya Temeke na baada ya hapo, saa kumi na mbili atatinga ndani ya Dar Live kuwaaga mashabiki wake.
“Kutakuwa na red carpet ambapo mashabiki wote watapata fursa ya kupiga picha na Samatta sambamba na kuzungumza naye mawili matatu kisha burudani kabambe itafuatiwa kutoka kwa Khalid Chokoraa ambaye tayari amemtungia wimbo, Twanga Pepeta chini ya Ali Chocky pamoja na Msagasumu,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa ni 5,000 kwa wote.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni