Pichani juu ni baadhi ya viongozi na wajumbe muhimu katika Mtandao wa Wanawake wa Katiba na Uchaguzi ukizungumza na vyombo vya habari kuainisha changamoto wanazokumbana nao wanawake na usawa kwenye siasa.
Kulia ni Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli (sasa ni Rais wa Tanzania) akihutubia katika mikutano yake ya kampeni 2015.
UCHAGUZI Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2015 uliokuwa na historia ya pekee kiushindani umemalizika tangu Oktoba 25, 2015. Kinachofanyika hivi sasa ni Serikali iliyoshinda chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuunda Serikali maeneo mbalimbali ili iweze kuwatumikia wananchi kwa miaka mitano na hasa kutekeleza miongoni mwa ahadi iliyozitoa kwa wapiga kura wake.

Pamoja na hayo, yapo mambo kadhaa ambayo yataendelea kukumbukwa katika mchakato wa uchaguzi huo. Kwanza ni msisimuko mkubwa na mwamko kwa takribani makundi yote ya jamii hasa vijana kushiriki kwenye uchaguzi huo. Kimsingi katika uchaguzi huo vijana walijitokeza kwa wingi kujiandikisha, kupiga kura na pia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia vyama anuai vya siasa vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Jambo la pili ni ushindani mkubwa uliokuwepo kati ya upande wa chama tawala na ule wa upinzani uliounganisha nguvu kiushirikiano, uliojipa jina la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ulioungwa mkono na vyama vya CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi na NLD ambavyo vilishirikiana kwa kuunganisha nguvu kwa kusimamisha mgombea mmoja nafasi ya urais.

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akihutubia katika moja ya mikutano yake ya kampeni.
Kwa mujibu wa takwimu za wapiga kura zilizotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva kabla ya uchaguzi; kundi la vijana walio na umri wa kati yaani miaka 18 hadi 35 lilikuwa na idadi kubwa ya wapiga kura.
Takwimu zilionesha wapiga kura vijana umri wa kati ya miaka 18 na 35 walikadiriwa kuwa ni asilimia 57 ya wapiga kura wote. Taarifa za NEC zinaonesha wapiga kura waliokuwa na umri wa zaidi ya miaka 50 ni asilimia 18 pekee, huku wengine asilimia 25 wakiwa na umri wa kati ya miaka 36 na 50. Hivyo hapo waweza kubaini namna ambavyo kundi la vijana lilivyoamua kujitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Lakini licha ya kundi hilo la vijana kujitokeza kushiriki uchaguzi na wengine kuomba kuchaguliwa changamoto pekee ilikuwa wao kuaminika na kuteuliwa ndani ya vyama vyao kabla ya kupewa nafasi ya kupeperusha bendera ya chama. Idadi kubwa walikwama ndani ya vyama vyao kutokana na urasimu uliokuwepo kwa baadhi ya vyama.

Na kwa wale waliofanikiwa kupita walikumbana na kikwazo kingine cha ushindani na ushawishi kwa wapiga kura ili waweze kushinda katika nafasi zote yaani kuanzia udiwani na ubunge kwenye maeneo yao. Mmoja ya vijana waliogombea kwa tiketi ya chama kimoja ambaye hakupenda jina lake litajwe katika makala haya anasema licha ya ushindani kuwa mkubwa na vikwazo vilikuwa ni vingi.
Anasema wapiga kura katika baadhi ya maeneo walizoeshwa na mfumo uliopita (viongozi wasio waadilifu) wa kushawishiwa na chochote ili waweze kukuchangua.
Anasema wapiga kura katika baadhi ya maeneo walizoeshwa na mfumo uliopita (viongozi wasio waadilifu) wa kushawishiwa na chochote ili waweze kukuchangua.
Anasema kwa wao ambao walishiriki bila kuwa na ushawishi wa namna hiyo walipata vikwazo vingi ikiwemo mikutano yetu kukosa wasikilizaji maana wanajua huwapi chochote.
Sehemu ya Mkutano wa kampeni za Mgombea wa Urais tiketi ya Chama cha CHADEMA ikiendelea kipindi cha uchaguzi 2015. CHADEMA kilishirikiana na vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi na NLD kwa baadhi ya nafasi katika uchaguzi huo.
"...Ilifikia mahali unafanya mkutano wa kampeni baada ya hapo baadhi ya wananchi wanakuuliza tumekusikiliza vya kutosha lakini unatuacha vipi...wanamaanisha uwape chochote (rushwa) kama hauna huwezi kuambulia kitu eneo hilo," anasema mgombea huyo kijana.
Lakini anaongeza zipo gharama nyingine za usafiri kwa timu ya kampeni kwa baadhi ya vijana na kugharamia vifaa vya mikutano ilikuwa ni kikwazo kingine kwa vijana waliojitokeza.
Lakini anaongeza zipo gharama nyingine za usafiri kwa timu ya kampeni kwa baadhi ya vijana na kugharamia vifaa vya mikutano ilikuwa ni kikwazo kingine kwa vijana waliojitokeza.
Kama kijana hana lasirimali fedha ilikuwa ni kikwazo kingine cha kufafikia wapiga kura na kueleza sera zako na chama chako. Wakati jambo hilo kwa wanasiasa wakongwe haikuwa tatizo kutokana na wao kuwa na uwezo kiasi kikubwa. Anasema katika vikwazo kama hivyo hauwezi kuuita ushindani sawa kwa makundi yote.
Hata hivyo kilio cha urasimu wa nafasi za vijana kwenye siasa kililikumba pia kundi la wanawake. Na katika kundi hili waweza kusema hali ilikuwa ni mbaya zaidi, maana licha ya mfumo dume kuendelea kuwatafuna ndani ya vyama uwezo wa kifedha katika kugharamia shughuli za siasa toka mchakato wa uteuzi hadi kampeni ilikuwa hali mbaya zaidi.
Magreth Mashenene ni mmoja wa akinamama aliyejitokeza kugombea nafasi ya udiwani Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza huku ikiwa ni mara ya kwanza kujaribu kuingia katika siasa za ushindani.

Anasema nia yake ilikuwa kutumia nafasi yake kushawishi uongezwaji wa bajeti katika sekta za afya, maji na miundombinu ya barabara, sekta ambazo ni changamoto kwa watu wanaoishi kata ya Shishani aliyogombea.
Magreth anasema wanawake wa sehemu hiyo ndiyo walikuwa waathirika wakubwa kwa kukosekana huduma za maji, kutunza jamaa na familia wanapougua na pia kwenye uchukuzi wa mazao kutoka mashambani kwenda kwenye masoko.
Baadhi ya mikutano ya kampeni za vyama vya upinzania ikiendelea kipindi cha kampeni 2015. Pichani ni chama cha CHADEMA kilichoshirikiana na vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi na NLD kwa baadhi ya nafasi katika uchaguzi huo.
Anasema gharama za kampeni bado ni changamoto kubwa kwa kundi hilo. Anasema kampeni za siasa nchini ni za gharama kubwa na ni changamoto kubwa kwa wagombea wanawake. Kwa sababu hiyo kuna haja ya kuwa na mikakati na mipango mingine ya kuwasaidia kutoka vyanzo mbalimbali ili waweze kukabiliana nazo.
Pamoja na uwepo wa vikwazo hivyo na changamoto nyingine kwa wanawake lakini bado kundi hilo lina idadi kubwa ya wapiga kura ukilinganisha na makundi mengine.
Pamoja na uwepo wa vikwazo hivyo na changamoto nyingine kwa wanawake lakini bado kundi hilo lina idadi kubwa ya wapiga kura ukilinganisha na makundi mengine.
Hivyo basi wanawake wana haki ya kujenga hoja ya uhalali wao wa kushiriki katika maendeleo ya Taifa na Serikali ina jukumu kubwa la kusawazisha uwanja wa ushindani na hususani kuweka taratibu kwa wagombea wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kufikia na kunufaika na rasilimali ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi.
Mfano takwimu zaonesha idadi ya wagombea wa nafasi za ubunge walioteuliwa katika Uchaguzi uliopita nchini nzima walikuwa ni wagombea 1,218, kati ya hao wanaume ni 985 na wanawake ni 233 huku idadi ya wagombea wa udiwani waliteuliwa nchi nzima walikuwa 10,879, kati ya hao wanaume 10,191 na wanawake 679. Kwa picha hiyo bado idadi ya kundi hilo ni dogo huku likiendelea kuathiriwa na vikwazo vilivyopo na changamoto.

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akihutubia njiani aliposimamishwa na wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, vyama vya siasa kwa kushirikiana na serikali bado vinajukumu la kuangalia namna ya kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo makundi ya vijana na wanawake kwa jumla na kuzitafutia ufumbuzi ili makundi hayo nayo yatoe wawakilishi wa kutosha huku kukiwa na ushindani ulio sawa katika siasa.
Pia baadhi ya mila na utamaduni katika jamii zinazombagua mwanamke na kumdharau kijana mwenye nia na ndoto ya kuongoza zipigwe vita.
Elimu ya uraia lazima iendelee ikiilenga zaidi jamii yenye kukumbatia mfumo dume, na hata kama kunauwezekano kuanzishwe mifuko maalumu ya fedha kuwasaidia wagombea wanawake na vijana hasa wale ambao wamejitosa kuingia kwenye siasa kwa mara ya kwanza ili kuwasaidia kumudu ushindani uliopo.

Imeandaliwa na Joachim Mushi wa www.thehabari.com
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni