Watu wapatao 50 wameuwawa katika
mlipuko karibu na eneo la kuabudia la dhehebu la Shia la Sayyid
Zeinab, kusini mwa Jiji la Damascus nchini Syria.
Kundi linalojiita Dola ya Kiislam
(IS) limesema kwenye mitandao ya kijamii kuwa limetekeleza shambulizi
hilo.
Eneo hilo ambalo ni la kiroho zaidi
kwa waumini Waislam wa dhehebu la Shia limewahi kushambuliwa hapo
kabla ambapo katika siku za karibuni ilikuwa Februari mwaka jana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni