.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 11 Januari 2016

WAZIRI KITWANGA AFANYA ZIARA JIMBONI KWAKE MISUNGWI, AWATAKA WANANCHI KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa Kata ya Kanyelele jimboni humo kabla ya kuanza mkutano wake na wananchi hao uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwakalima. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo cha Shule ya Sekondari Kanyelele ambapo kimeharibika. Hata hivyo, aliwataka wananchi hao waweke utamaduni wa kuchangia maendeleo ya vijiji vyao. Picha zote na Felix Mwagara.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (wapili kushoto) akimuuliza swali Diwani wa Kata ya Kanyelele, Paschal Kilangi (kulia) wakati Mbunge huyo alipokuwa akikiangalia choo cha Shule ya Sekondari Kanyelele jimboni humo kilichobomoka. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho na kuwaomba wananchi wa kata hiyo waanze kuchanga kwa kasi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (wapili kushoto) akiwa na Diwani wa Kata ya Kanyelele, Paschal Kilangi (kushoto) pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kanyelele, Kudehwa Gapi (wapili kulia) wakiwa wanaikagua shule hiyo ambayo choo chake kilikuwa kimebomoka kwa kudidimia chini ya ardhi. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho na kuwaomba wananchi wa kata hiyo waanze kuchanga kwa kasi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akikiangalia kikundi cha burudani cha Kijiji cha Mwakalima kilichokuwa kinatumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Kata ya Kanyelele jimboni humo. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo cha Shule mya Sekondari Kanyelele kilichoharibika na kuwaomba wananchi wa Kata hiyo waanze kuchangia kwa kasi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akizungumza na wananchi wa Kata ya Kanyelele katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwakalima jimboni humo. Waziri Kitwanga kabla ya mkutano huo alikikagua choo cha Shule ya Sekondari Kanyelele kilichobomoka na alichangia shilingi laki tano pamoja na kuwataka wananchi wa kata hiyo kuchangia fedha zaidi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.
Diwani wa Kata ya Kanyelele, wilayani Misungwi, Paschal Kilangi akiwaonyesha wananchi shilingi laki tano alizotoa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa choo cha Sekondari ya Kanyelele kilichobomoka shuleni hapo. Waziri Kitwanga aliwaomba wananchi wa kata hiyo kuhakikisha wanatoa michango zaidi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.
Mtendaji wa Kijiji cha Mwakalima, Kata ya Kanyelele, wilayani Misungwi, Samson Ngalula akisoma risala kwa niaba ya wananchi kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kushoto) hajaanza kuzungumza na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwakalima kijijini humo. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo cha Shule mya Sekondari Kanyelele kilichoharibika na kuwaomba wananchi wa Kata hiyo waanze kuchanga kwa kasi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka. Picha zote na Felix Mwagara.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni