.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 31 Januari 2016

WAZIRI MAKAMBA ATOA MSAADA MABATI 300 KWA WAHANGA AMBAO NYUMBA ZAO ZILIZOEZULIWA NA UPEPO JIMBONI KWAKE

                                                                                           NA RAISA SAID,BUMBULI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshugulikia Muungano na
Mazingira,January Makamba ametoa msada wa mabati 300 kwa wananchi
ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa
iliyonyesha maeneo mbalimbali jimboni humo.

Nyumba hizo zilikuwa 40 ikiwemo Kanisa na Msikiti zimeezuliwa mapaa
katika kijiji cha Msamaka kilichopo wilayani Bumbuli kufuatia Mvua
kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha.

Mvua hiyo imesabisha kaya hizo kukosa mahali pa kuishi , huku wengi wa waathirika wakipewa hifadhi kwenye nyumba za majirani zao.

Akizungumza na waandishi wa habari hapo Jana Afisa Mtendaji wa kijiji
cha Msamaka Mbazi Shemhando alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo
January 27 mwaka huku saa kumi jioni.

Alitaja sehemu zilizo athirika zaidi kuwa ni Vitongoji vya Kwemchaa, Nazareti,CCM, Kwakorosi pamoja na kitongoji cha Kwamingojo ndio vimeweza kuathirika na maafa hayo.

Hata hivyo aliongeza kuwa waathirika watukio hilo Kwa sasa wamehifadhiwa kwenye nyumba za Jirani wakati utaratibu mwingine wa kuwasaidia ukiendelea kuwekwa.

Akikabidhi msaada huo Makamba alisema kuwa kutokana na tukio hilo
anatanguliza msaada huo kwanza wakati akiendelea kutafuta msaada zaidi.

"Nimejikusanya Kwa hiki kidogo ili kiweze kusaidia pale penye uhitaji Kwa haraka wakati tukiendelea na utaratibu mwingine" alisema Makamba

Makamba aliwataka wananchi wote kupanda miti ili kuepuka upepo mkali unaosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo tofauti

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni