.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 5 Januari 2016

WAZIRI MKUU AFUNGUA TAWI LA BENKI YA POSTA SONGEA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungungua tawi la Benki ya Posta la Songea akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Januari 4, 2016. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Uratibu, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama .

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefungua tawi la Benki ya Posta iliyopo mjini Songea, wakati akiwa katika ziara mkoni Ruvuma inayotarajiwa kumalizika jumatano wiki hii.

Akizungumza na uongozi na wafanyakazi wa Benki ya Posta pamoja na wateja waliohudhuria ufunguzi wa tawi hilo uliofanyika nje ya benki hiyo hapo jana, Waziri Mkuu amesema amefarijika kuona benki hiyo iliyokua imekumbwa na matatizo sasa imezaliwa upya na kumpongeza Mkurugenzi wa Benki ya Posta nchini Bwana. Sabasaba Mushindi kwa jitihada zake za kufufua benki hiyo.

Amesema, Benki hiyo inalenga wananchi wenye vipato vya chini, SACOSS, Vyama Vya Ushirika na wafanyabiashara wadogo wadogo , nakusisitiza kuwa wafanyabishahara na wananchi wa Ruvuma wanaweza kukopa ili kukuza mitaji yao lakini waweze kurudisha mikopo hiyo ili iwanufaishe na wengine.

Waziri Mkuu Majaliwa, pia amefurahishwa na huduma ya mikopo kwa wasataafu inayotolewa na benki hiyo, ambapo amesema amefarijika kuona wazee nao wana nafasi ya kukopa kupitia benki ya posta.
Pia, ametumia fursa hiyo kutoa wito wa kuwataka watanzania kuacha tabia ya kutembea na fedha nyingi mifukoni kwani hukaribisha wizi na kusababisha matumizi yasiyo na mpangilio.

“Watanzania tubadilike , ni muhimu sasa watanzania kubadilika tuhifadhi fedha zetu Benki” alisema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake,Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta nchini Bwana. Sabasaba Mushindi amempongeza Waziri Mkuu na Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kuchaguliwa na wananchi na namna ambavyo wameendelea kuingoza Serikali chini ya kauli mbiu ya HAPA KAZI TU.

Bwana. Mushindi amesema benki ya Posta ilianzishwa miaka 90 iliyopita ikiwa chini ya utawala wa kikoloni, ina lengo la kuchochea utamaduni wa kujiwekea akiba kwa watanzania, takwimu zikionesha watanzania wako nyuma katika kuweka akiba.

Chini ya 10% ya mapato ndio yanawekwa kama akiba, na 14% ya watanzania wanaohifadhi fedha benki, na 3% tu ya watanzania wana sifa na uwezo wa kukopa benki.

Aidha, amesema baada ya kukabiliana na changamoto mbalimbali hivi sasa benki ya Posta inaendelea kuimarika ambapo wamekua wakipata faida na baada ya mahesabu kukamilika wanatarajia kupata hadi kiasi cha bilioni 12 kwa mwaka 2015.

“Hadi sasa 70% ya matawi ya benki yamefanyiwa ukarabati, kumekuwepo na huduma kama PPT popote, akaunti ya michezo (Sports account) ambayo imesaidia vilabu mbalimbali kama Mbeya City na Stand United ya Shinyanga, pia benki imetoa kiasi cha shilingi milioni 150 kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii ” alisema Bwana. Mushindi

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, JANUARI 5, 2016.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni