Mchezo wa kirafiki baina ya Uholanzi na Ufaransa ulisimama
katika dakika ya 14 na kukaa kimya kwa dakika moja kwa ajili ya
kumbukumbu ya mchezaji maarufu wa nchi hiyo Johan Cruyff aliyefariki
dunia.
Mchezaji huyo wa zamani wa klabu za Ajax na Barcelona, ambaye
alikuwa maarufu akivalia fulana namba 14 mgongoni, alifariki kwa
ugonjwa wa saratani Alhamisi, akiwa na umri wa miaka 68.
Katika mchezo huo Uholanzi ilibidi wapambane kiume wakiwa nyuma
kwa mabao 2-0 katika kipindi cha kwanza na kusawazisha baadaye hata
hivyo Blaise Matuidi aliipatia Ufaransa bao la tatu katika dakika za
mwisho na kufanya matokeo kuwa 3-2.
Olivier Giroud akiachia mkwaju uliojaa wavuni na kuandika bao la pili la Ufaransa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni