.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 24 Mei 2016

KASESELA AWATEMBELEA WAJASIRIAMALI MJINI IRINGA

Mkuu wa wilaya Iringa, Richard Kasesela akiangalia moja ya viatu katika duka la mmoja wa vijana wajasiriamali mjini Iringa. 

Mkuu wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alitembelea maduka ya vijana wajasiriamali waliofungua maduka ili kuweza kunyanyua maisha yao.

Vijana hawa wamepata mikopo na kuweka maduka yao katika hadhi ya kimataifa. Akizungumza nao Kasesela alifurahishwa sana na unadhifu wa maduka hayo yaliyopo mtaa wa msikiti wa miyomboni. 

Kasesela hutumia jumapili kutembelea wafanya biashara ndogondogo na wale wa sokoni ili kuwahamasisha kukuza biashara zao na kuitangaza. 

Maduka haya yana wiki moja tu tu toka yaanzishwe hayana tofauti na yale ambayo ukienda nje ya nchi utayakuta. Wajasiliamali walialamikia wingi wa kodi ndogo ndogo pia mazingira ya baishara bado si rafiki sana. Mkuu wa wilaya aliahaidi kulifanyia kazi.
Mkuu wa wilaya Iringa, Richard Kasesela akiongea na mmoja wa vijana wajasiriamali katika duka lake la nguo na viatu mjini Iringa.





Hakuna maoni :

Chapisha Maoni