MKUU WA WILAYA ya Iringa Mh Richard Kasesela aliongoza kikosi cha wana nchi na maafisa wa wanyama pori kumsaka Kiboko aliyevamia mazao ya wananchi na kutishia maisha ya wananchi katika kijiji cha Magunga tarafa ya Kiponzelo.
Kiboko huyo alijificha kwenye eneo oevu amabapo wananchi wa kijiji hicho waliogopa kutembea kufanya shughuli za kilimo.
Mnamo saa 10 na nusu jioni kiboko huyo alipataikana na kuuawa na baadae wananchi kugawiwa nyama yake. Ilikuwa kazi ngumu kumtoa kwenye dimbwi alilo angukia baada ya kuuawa kwa risasi. Kumekuwa na matukio ya wanyama wa porini kuvuka mbuga na kuingia vijijini. wiki mbili zilizo pita simba alionekana kijiji cha Idodi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni