Jumanne, 31 Mei 2016
MKE WA RAIS MAMA JANETH AWATAKA WATANZANIA KUWASAIDIA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkaribisha Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa Ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam. Mama Majaliwa alifika Ofisini hapo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na mke wa Rais.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli Magogoni jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimuonesha Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa mafuta maalumu yanayotumiwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino ambayo atayagawa hivi karibuni kwa baadhi walemavu wa ngozi katika maeneo mbalimbali nchini. Pia Mke wa Rais mama Janeth amewaomba watanzania kuwajali Wazee na watu wenye ulemavu wa ngozi. PICHA NA IKULU
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni