






Baadhi ya waandaji wa mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja.
Baada ya kufanyika nchini kwa miaka 10, mradi wa SCMS ambao ulikuwa ukisimamiwa na John Snow Incorporated (JSI) kwa ushirikiano na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) limeiahidi serikali ya Tanzania kuwa litaendelea kuisaidia katika misaada mbalimbali ya afya licha ya kumalizika kwa mradi huo.
Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi wa USAID nchini, Tim Donnay katika mkutano ambao ulikutanisha wadau mbalimbali wa afya ili kujadili mradi wa SCMS ambao umefikia tamati baada ya kufanyika nchini kwa miaka 10.
Bi. Donnay alisema serikali ya Marekani kupitia USAID imejipanga kuendelea kuisaidia Tanzania katika sehemu mbalimbali ambazo zinahusu Afya.“USAID itaendelea kuisaidia Tanzania ili kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya upatikanaji wa huduma bora wa kiafya ... kumalizika kwa mradi huu hukutafanya kusitishwa kwa huduma ambazo zinatolewa kwa sasa,” alisema Bi. Donnay.
Nae mgeni rasmi katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Mpoki Ulisubya alisema kufanyika kwa mradi huo nchini kumewezesha kusaidia kuboreshwa kwa kasi huduma za afya tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
“Mradi huu umetusaidia sana awali hata utolewaji wa dawa kwa waathirika wa UKIMWI ulikuwa ni laki na nusu kwa mwaka ila kwa sasa kuna upatikanaji wa dawa hadi laki nane kwa mwaka,“Mbali na hiyo pia wametujengea maghala ambayo yanatumika kuhifadhi dawa na hata kusaidia kuweza kuwasogezea huduma wananchi ambazo awali hazikuwa zikitolewa,” alisema Ulibusya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni