Leo ni siku muhimu sana kwangu maana inanikumbusha siku niliyoletwa Duniani na Mungu kupitia Mama yangu kwa kusudi maalumu hapa duniani.
Napenda Kumshukuru Mungu kwa maana neema na rehema zake ni Za milele. Nasema asante kwa kunifanya kuongeza mwaka mwingine huku nikiwa na afya njema.
Kiukweli Sina cha Kumlipa Mwenyezi Mungu zaidi ya Kumsifu na Kumwabudu yeye kwa maana Sio kwa uwezo wangu.Napenda kuwashukuruni wote Ambao Mmekuwa mkiniombea na kunitakia heri ya kuzaliwa kwangu Nasema asante na Mungu awabariki sana.
Nakukabidhi wewe bwana njia zangu na kukutumainia kwasababu umeagiza kila akukabidhie njia zake na kukutumainia unaenda kumtendea. Zaburi 37: 5 Leo nasema asante sana kwa Maana kila napokuita Wewe unaitika.
Naomba pia uendelee kuziimarisha hatua zangu kwa maana uliagiza katika Zaburi 37:23 Kuwa "Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake"
Hakika wewe ni Mungu wa Wote. Nachukua fursa hii kuwa shukuruni wote Ambao mmenitakia baraka na heri katika siku hii muhimu sana kwangu ambayo inanifanya nitafakari matendo yangu hapa duniani, Uhusiano wangu na Mungu wangu, Uhusiano wangu na Ndugu zangu, Uhusiano na Jamii yangu pamoja na rafiki zangu hakika Namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kupatana na Ndugu zangu, jamii yangu na hata marafiki zangu.
Kiukweli Namshukuru Mungu kwasababu Ni kwa neema zake na Rehema zake ndio zimenifikisha hapa wala sio kwa ujanja wangu wala mimi sio mwema sana kuzidi wengine.
Wewe Ni Mungu wa wote, Huchelewi wala Huwahi Hakika nitakusifu na kukuabudu siku zote za maisha yangu kwa maana matendo yako makuu uliyonitendea Nayaona na kuyafurahia.
Asante sana Mungu wangu naomba uendelee Kutimiza haja za Moyo wangu. Nitaendelea Kukushangilia na Kukusifu kwa maana kila napokuita unaitika.
Happy Birthday to You Josephat Lukaza - Lukaza Blog
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni