Timu ya taifa ya Hungary
imewashangaza watu katika michuano ya Euro 2016 baada ya kupata
ushindi dhidi ya Austria waliobakia na wachezaji 10 katika mchezo wao
wa kwanza katika michuao hiyo.
Katika mchezo huo Austria
walikaribia kufunga goli la mapema mno katika michuano hiyo lakini
shuti la David Alaba katika sekunde ya 28 liligonga mwamba.
Hungary waliwadhibiti vyema
wapinzani wao Austria kwa kuongoza wakati Adam Szalai akiunganisha
pasi ya Laszlo Kleinheiser na kupachika goli la kwanza na kisha
Zoltan Stieber kufunga goli la pili baadaye.
Adam Szalai akiifungia Hungary goli la kwanza katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni