Jumanne, 14 Juni 2016
KATIBU MKUU RWEGASIRA AWAVISHA VYEO VYA MRAKIBU MSAIDIZI WAHITIMU 98 WA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi ngazi ya juu na kuwatunuku Maafisa Magereza 98 Cheo cha Mrakibu Msaidizi. Katika hotuba yake Katibu Mkuu aliwaasa wahitimu hao wakaitumie taaluma walioipata chuoni hapo kwenda kuwahudumia Watanzania kwa uadilifu. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Minja, akihutubia wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi ngazi ya juu na kuwatunuku Wahitimu 98 wa Cheo cha Mrakibu Msaidizi. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Gwaride la Maafisa Wahitimu wa kozi ya Uongozi ngazi ya Juu wa Jeshi la Magereza likijiandaa kupita mbele ya Jukwaa la Mgeni kwa heshima kama wanavyoonekana wakiwa wakakamavu katika picha. Sherehe za kufunga Mafunzo hayo zimefanyika leo Juni 14, 2016 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania kilichopo Ukonga, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua Gwaride la Wahitimu kama inavyoonekana katika picha.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akimvisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi za juu aliyefanya vizuri katika masomo ya Medani kwa niaba ya Wahitimu wote wa kozi hiyo(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akishuhudia tukio hilo la uvishaji cheo.
Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wageni Waalikwa kutoka Taasisi mbalimbali wakifuatilia kwa karibu Gwaride la Wahitimu.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi juu ya Uendeshaji wa Jeshi la Magereza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani).
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kulia) akimuongoza Mgeni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira kuelekea eneo la hafla ya kufunga rasmi Mafunzo ya Uongozi ngazi za juu wa Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, ACP. Erasmus Kundy(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni