Rais
Uhuru Kenyatta amewahutubia wakenya katika maadhimisho ya Siku ya
Madaraka Mjini Nakuru na kuwataka kuwahofia viongozi wanaotaka
kukiuka Katiba ili kufanikisha agenda zao binafsi.
Rais
Kenyatta amesema viongozi lazima waheshimu taasisi zote zilizowekwa
na Katiba kuanzia uongozi wake na namna zinavyoendesha shughuli zake
nchini, kauli ambayo inaonyesha kuwalenga wapinzani wanaotaka ivunjwe
tume ya uchaguzi IEBC.
Wakati
huo huo katika mkutano mwingine wa Siku ya Madaraka Jijini Nairobi,
kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema hakutakuwapo uchaguzi mkuu
mwaka 2017 iwapo maafisa wa sasa wa tume ya uchaguzi hawatoondoka.
Wakihutubia
maelfu ya wafuasi wake Uhuru Park, Raila na Moses Wetangula wamesema
watataja majina ya wawakilishi wao kesho, watakaoungana na serikali
katika mazungumzo kuhusina na mvutano wa uwepo wa tume ya uchaguzi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni