Mshauri wa Mahakama ya Ulaya amesema
kuwa kampuni nchini Ulaya zitaruhusiwa kuzuia uvaaji wa vazi la
hijabu ama kitambaa cha kichwani makazini, iwapo tu watazuia alama
zote za kidini na za kisiasa katika maeneo ya kazi.
Mshauri huyo wa Mahakama ya Sheria
ya Ulaya, iwapo alama za kidini zinazoonekana na za kisiasa zitapigwa
marufuku katika sera ya mavazi kazini, basi vazi la hijabu nalo
lipigwe marufuku pia makazini.
Mshauri huyo Mwanasheria Mkuu
Juliane Kokott amesema iwapo mwajiriwa hawezi kuicha jinsia yake,
asili yake, umri wake ama ulemavu wake aingiapo kwenye mlango wa
ofisi, basi yeye naye hawezi kudhibiti imani za watu katika maeneo ya
kazi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni