.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 13 Juni 2016

MKUTANO MKUBWA WA OYES 2016 WAANZA KATIKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

Umati wa wananchi wa Jiji la Mwanza ukifuatilia mahubiri ya Mwimbaji na Mhubiri JJ.Rwiza wakati akihubiri jana katika ufunguzi wa Mkutano wa Open Your Eyes and See OYES 2016 unaofanyika katika Viwanja vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Mkutano wa OYES 2016 ulianza jana June 12,2016 na unatarajia kufikia tamati jumapili ijayo June 19,2016 ambapo kila siku utakuwa ukianza majira ya saa nane mchana. Ni Mkutano mahususi kwa ajili ya kuwafungua watu wote wenye uhitaji ambao kwa muda mrefu wameteseka na vifungo vya ibirisi.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola (Kushoto), akimkaribisha Mwimbaji na Mhubiri JJ.Rwiza kuhubiri katika Mkutano wa Open Your Eyes and See OYES 2016.
Mwimbaji na Mhubiri JJ.Rwiza akihubiri katika Mkutano wa Open Your Eyes and See OYES 2016 unaofanyika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.

Bonyeza Hapa Kujua Zaidi Kuhusu OYES 2016 


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni