Watu
50 wamethibitishwa kufa katika tukio la shambulizi la silaha kwenye
klabu ya usiku ya mashoga huko Orlando, Florida, huku hali ya
tahadhari ikitangazwa kwenye mji huo na Meya Buddy Dyer.
Mtu
huyo aliyekuwa na silaha ametambulika kama Omar Mateen, naye aliuwawa
baada ya kuwashikilia watu mateka. Watu wengine 53 wamejeruhiwa
kwenye tukio hilo katika klabu ya Pulse.
Tukio
hilo la shambulizi la kutumia silaha ni baya kuwahi kutokea katika
historia ya Marekani, ambapo tayari polisi wamesema ni tukio la
kigaidi lililotokana na misukumo ya kiimani.
Polisi akiwa amevalia nguo za kazi katika eneo la tukio la kigaidi huko Orlando, Florida Marekani
Mshambuliaji aliyeuwawa Omar Mateen akiwa amepozi akijipiga picha za Selfie kwa kutumia simu na kioo.
Watu waliopatwa na mshtuko baada ya kutokea tukio hilo la shambulizi la kutumia risasi katika klabu ya Pulse.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni