Mahakama
nchini Qatar imemtia hatiani mwanamke mmoja Mdachi, kwa kufanya ngono
bila ya kuolewa baada ya kuwaambia polisi wa nchi hiyo amebakwa.
Mwanamke
huyo mwenye umri wa miaka 22, amehukumiwa kifungo cha nje na amepigwa
faini ya dola 824, na pia atalazimika kuondoka Qatar kwa nguvu.
Wakili
wake amesema mteja wake alikunywa pombe akiwa hotelini Doha mwezi
Machi na kuamka asubuhi akajikuta kwenye ghorofa asilolitambua na
ndipo alipobaini kuwa kabakwa.
Mtuhumiwa wa ubakaji alyedai
waliridhiana kufanya ngono, amehukumiwa kupigwa bakora 100, kwa
kufanya ngono nje ya ndoa. Pia atachapwa fimbo 40 kwa kunywa pombe.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni