Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini
Oscar Pistorius ametembea kwa taabu Mahakamani akitumia sehemu ya
miguu yake iliyobakia katika kujaribu kumshawishi Jaji kuwa yeye ni
dhaifu mno kuweza kumuua kwa makusudi mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Mwanariadha huyo anayetumia miguu
maalum ya kukimbilia, alitakiwa kuvua miguu yake bandia, na kubakia
na miguu yake iliyobakia wakati wa kesi yake iliyokuwa ikirushwa moja
kwa moja kwenye runinga.
Oscar Pistorius akisimama kwa kutumia sehemu za miguu yake iliyobakia
Oscar akijikaza na kutembea kwenye chumba cha mahakama
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni