Kaimu Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mchana huu wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa na mwandishi wa ” The Ecomist” Gazeti la Kiingereza linatoka kwa wiki dhidi ya Serikali ya Tanzania. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TCI), Daud Biganda.
Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TCI), Daud Biganda (kulia), akitoa ufafanuzi wa Uchumi tangu Rais Dk. John Magufuli aingie madaraka na miradi iliyosajiliwa na kituo hicho.
Taarifa akichukuliwa na wanahabari.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Kiingereza linalotpka kila wiki lililodai kuwa Rais Dk.John Magufuli anaongoza nchi kwa msukumo licha ya kuonekana mzuri na kuwa taarifa hiyo imelenga kuupotosha umma.
Habari iliyoandikwa kwenye gazeti hilo ilikuwa na kichwa kilicho andikwa “Government by gesture, A President who looks good but governs impulsively”
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa ufafanuzi wa habari hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa alisema taarifa hiyo haikuwa na uzalendo na amewataka wanahabari kuwa makini na habari zenye mlengo wa kupotosha taifa.
“Nawaombeni wanahabari wenzangu kuweni makini na taarifa zenye mlengo wa kupotosha umma” alisema Zamarad.
Akitoa ufafanuzi kuhusu suala la uchumi Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Daud Biganda alisema taarifa hiyo siyo sahihi na imelenga kupotosha na inavuruga ukweli kwani Tangu Rais Dk.John Magufuli aingie madarakani kwa kipindi cha kati ya mwezi Desemba 2015 na 2016, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeweza kuandikisha miradi ya uwekezaji ipatayo 551 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 9,211.88 kati ya miradi hiyo miradi 229 yenye asilimia 42 inamilikiwa na watanzania, miradi 215 yenye asilimia 39 inamilikiwa na wageni na miradi 107 yenye asilimia 19 inamilikiwa kwa njia ya ubia kati ya watanzania na wageni.
Biganda alisema kuwa miradi yote hiyo ya uwekezaji ilitarajiwa kuzalisha ajira zipatazo 55,970 na kuleta matokeo mengine kwa watanzania na kuwa imesajiliwa na TIC.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni