Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kuwafahgamisha
wanachama wa Young Africans na familia ya mpira kwa ujumla kuwa
mchakato wa uchaguzi wa Klabu ya Young Africans unaendelea vizuri na
unasimaiwa na Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho kwa mujibu wa utaratibu
ulioutoa awali.
Fomu za uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa katika ofisi za Makao Makuu
ya TFF-Karume. Vilevile fomu zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya TFF
amayo ni www.tff.or.tz.
TFF inafuatilia kwa karibu mwenendo mzima wa mchakato na taarifa zote
zitatolewa na TFF kupitia wasemaji wake na Mwenyekiti wa Kamati ya
Uchaguzi ambaye ni Wakili Msomi, Alloyce Komba.
Tayari Kamati ya Uchaguzi ya TFF, iliyopewa jukumu la kusimamia
uchaguzi wa Klabu ya Young Africans imeridhishwa na mwenendo wa
wanachama kwa namna wanavyochukua na kurejesha fomu.
Na kutokana na mipango yake, imesogeza mbele mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu mpaka Jumatatu Juni 6, 2016 saa 10:00 jioni.
Hadi sasa wanachama tisa (9) wamechukua na kurejesha fomu. Wanachama
hao ni Aaron Nyanda na Titus Osoro wanaowania nafasi ya makamu
mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 inayotambulika serikalini
hadi sasa.
Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu
Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar.
Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 25, 2016.
Fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu
ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili
fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho www.tff.or.tz
Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya
mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya
ujumbe wa kamati ya utendaji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni