Mbwana Samatta ( kushoto ) akitarajiwa kuwasili usiku wa Juni 1, 2016 kutoka Genk Ubelgiji, tayari Thomas Ulimwengu ( kulia ) kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amejiunga na kambi ya timu ya soka ya Tanzania- Taifa Stars.
Na katika hatua nyingine, Uongozi wa Bia ya Kilimanjaro inayozalishwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL), unatarajia kutembelea timu ya Taifa Stars kesho Alhamisi Juni 2, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo kabla ya kuivaa Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Maataifa ya Afrika (AFCON).
Mchezo huo utasimamiwa na Waamuzi wanne kutoka Gabon, ambao ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric. Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF) na Misri imetua alfajiri ya leo Juni 1, 2016 na imeweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.
Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jana Mei 30,2016 ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars. Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni