Ni kawaida kabisa kuwaona wanawake
wakipoteza muda mwingi kupekua kabati wakijaribu kufikiria nguo gani
ya kuvaa kiasi hata ya kuwafanya kuwa katika hali ya kupaniki.
Watafiti wameamua kufuatili muda
wanaotumia wanawake kutafuta nguo ya kuvaa na kubaini hutumia karibu
dakika 17 kwa siku, sawa na siku nne kwa mwaka wakitafuta nguo
kabatini.
Hali hiyo ya wanawake kutumia muda
mwingi kutafuta nguo ya kuvaa kabatini hufanya moja kati ya wanawake
10 kuchelewa kazini na moja kati ya 20 hushindwa kufika kwenye hafla
kabisa.
Asilimia 21 ya wanawake wamekiri
kuwa kitendo cha kuhangaika kuchagua nguo ya kuvaa kabatini
huwasababishia ugomvi na wenza wao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni