Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Haki Ardhi Yelfred Mienzi akiendelea kutoa kutoa mada katika mkutano huo
Mmoja wa washiriki akichangia mada katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa lush garden jijini hapa
Wadau wa masuala ya ardhi kutoka taasisi zisizo za kiserikali wamesema mchakato unaoendelea hivi sasa wa kuainisha mapendekezo ya mabadiliko ya sera ya ardhi nchini unapaswa kutumika vizuri kwa wadau wote kwa kutoa maoni yatakayosaidia kupata sera iliyobora ili kuondoa migogoro ya ardhi iliyokithiri katika maeneo yote nchini.
Wadau hao wamesema hayo jijini hapa katika mkutano uliowakutanisha wataalamu kutoka Taasisi hizo kwa lengo la kupitia maoni yaliyo tolewa na Taasisi zote za kiraiya na kupata mapendekezo ya jumla yatakayowasilishwa serikali ni.
Wataalamu wa ardhi kutoka taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali nchini wamekutana jijini ARUSHA kwa lengo la kupitia maoni yote yaliyoanishwa na Taasisi hizo ili waweze kupata mapendekezo ya jumla yatakayo wasilishwa serikalini kwa lengo la kuboresha sera ya ardhi.
Wamesema kuwa bado jamii haijashiriki vya kutosha kulingana na matizo yaliyopo, ambapo ni vema wadau wote wakatumia nafasi iliyotolewa na serikali kutoa maoni yao ya kutosha juu ya sera hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Haki Ardhi Yelfred Mienzi alisema kuwa zipo changamoto nyingi katika masuala ya ardhi zinazohitaji jamii kushiriki kwa mapana kutoa mawazo yao ili waweze kuisaidia serikali kutoa sera itakayotatua migogoro iliyokithiri katika maeneo mbalimbali nchini haswa vijijini na mjini.
"unajua hii ni fursa ya wananchi kutoa maeneo yao juu ya sera hii ya ardhi kama m navyosumbuliwa ardhi ni kila kitu sasa iwapo tunatatoa maoni yetu Vibaya sisi ndio tutakuwa, unajua aya maoni yetu yakupelekwa ndio yanatengeneza sera sasa sera inaweza kuwa nzuri kwetu iwapo itakuwa nzuri na itakuwa mbaya kwetu iwapo tutaboronga"alisema Mienzi.
Naye Mwakilishi kutoka chama cha wanasheria wanaotetea haki za Wanawake Tanzania, Naseku Kisambu alisema kuna umuhimu wa kuipitia sheria ya ardhi kwa kina ili iweze kutoa haki kwa Wanawake hasa katika umiliki wa ardhi kutokana na wao kunyimwa haki kwa muda mrefu sasa.
Alisema kuwa katika sheria ya ardhi iliopita amna sehemu inapoainisha kuwa mtoto wa kike anaweza kupewa umiliki Shi wa ardhi, hivyo nivigumu mwanamke kumiliki ardhi labda ukute kazawadi wa au kununua mwenyewe hivyo watatumia fursa hii ya kuchangia sera hii ili kutoa mapendekezo ya kusaidia mwanamke kumiliki au kumilikishwa ardhi.
Gazeti hili liliongea na Mkurugenzi mtendaji wa chama cha Waandishi wa habari za mazingira Tanzania John Chakomo naye alisema ni vizuri makundi yote yanayotoa maoni yao, yakatoa mapendekezo yatakayoifaidisha jamii yote bila kupendelea makundi yao wanayoyatetea.
Alisema kuwa iwapo haki na sheria ikifuatwa ya kukusanya maoni basi itasaidia kupata sera nzuri itakayo mlenga kila mwananchi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa taasisi ya CARE, Mery Ndalu, amesema tayari asasi mbalimbali wameshatoa maoni yao ambapo mkutano huo umeyapitia na sio kupitia tu basi watayaboresha ili waweze kutoa mapendekezo yatakayoisaidia serikali kutengeneza sera itakayoleta tija kwa wananchi.
Aidha alisema kuwa wanatarajia kupeleka mapendekezo yatakayosaidia kuboresha haki za umiliki ardhi wa kimila ili kutoa fursa kwa jamii ya watu wachini kufaidika na ardhi yao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni