.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 1 Juni 2016

WAZIRI WA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO ATEMBELEA MAGHALA YA KUHIFADHIA VYAKULA KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

MENEJA Mkuu wa kampuni ya Evergreen Abdulghafar Ismail Mohammed akimfahamisha Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali juu ya hali ya chakula nchini alipotembelea katika ghala lake Saateni mjini Zanzibar.
BAADHI ya vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen Saateni mjini Zanzibar.
MENEJA Mkuu wa kiwanda cha Zanzibar Miling Corporation Khalid Ali Yussuf, akimpa maelezo Waziri Amina Salum Ali juu ya uzalishaji wa chakula alipotembelea ofisini kwake Mtoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akiwa katika maeneo ya kiwanda cha Zanzibar Miling Corporation Mtoni alipofanya ziara maalum kwa ajili ya kuangalia hali ya chakula nchini wakati huu wa kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan
WAZIRI Amina Salum Ali akiangalia vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen lililopo Saateni mjini Zanzibar.
WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kiwanda cha Zanzibar Milling Corporation kilichoko Mtoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akioneshwa ngano na Meneja Mkuu wa kiwanda cha Zanzibar Milling kilichoko Mtoni Zanzibar Khalid Ali Yussuf, katika sehemu ya usagishaji alipotembelea kiwanda hicho.
MENEJA Mkuu wa kampuni ya Bopar Enterprises Said Nassir Said, akizungumza na Waziri Amina Salum Ali wakati Waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake Mombasa mjini Zanzibar.
 

                PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni