









Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog kanda ya Kaskazini.
Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi uliyoko wilayani Kahama, katika mkoa wa Shinyanga, umekabidhi kwa uongozi wa katika Halmashauri ya mji wa Kahama majengo ya shule mpya ya msingi Budushi yenye madarasa sita, ofisi ya walimu na nyumba moja ya walimu yenye uwezo wa kuishi familia mbili.
Akikabidhi madarasa hayo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa Mwaipopo amesema ujenzi huo umefadhiliwa na Mgodi wa Buzwagi kwa zaidi ya shilingi milioni mia nne na themani kupitia mfuko wa Acacia Maendeleo Fund, ambao umelenga kuwapunguzia adha wanafunzi wa eneo hilo la Budushi na maeneo yanayozunguka eneo hilo kuondokana na adha ya kutembea mwendo mrefu kwenda shule.
Aidha, Meneja mkuu huyo wa Mgodi wa Buzwagi alikabidhi pia nyumba mbili za kisasa za walimu zenye uwezo wa kuishi familia nne kwa shule ya msingi Mwime hatua ambayo amesema kuwa itasaidia katika kupunguza tatizo la nyumba kwa walimu kwa shule hiyo. Nyumba hizo ambazo zimejengwa kwa kutumia teknolojia ya Tofali za kufungamana zimegharimu shilingi milioni mia mbili arobaini na nane (248,126,000/=)
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkurlu aliyepokea miradi hiyo ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutekeleza miradi ya Maendeleo”
Akizungumza kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Abel Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuiletea Jamii Maendeleo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni