Magoli
yaliyofungwa na Diego Costa, Oscar, Eden Hazard na Pedro yameipatia
Chelsea ushindi katika mechi ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya
Werder Bremen ya Ujerumani, hata hivyo kocha Antonio Conte bado
anashida ya ukuta wa timu yake.
Katika
mchezo huo Chelsea ilipata magoli mawili ndani ya dakika 10 za mwanzo
wa mchezo huo kupitia kwa Hazard na Oscar na kuwafanya waongoze kabla
ya Claudio Pizarro kuchomoa goli moja kwa mkwaju wa penati.
Katika
kipindi cha pili Diego Costa aliifungia Chelsea goli la tatu na
baadaye mchezaji wa Werder Bremen, Lennart Thy alifunga goli la
pili, lakini mambo yalizidi kuwa magumu pale Pedro alipofunga goli la
nne katika dakika za mwisho.
Eden Hazard akiachia shuti lililoandika goli la kwanza kwa Chelsea
Diego Costa akiachia shuti lililoandika goli la tatu la Chelsea
N'Golo Kante akiwania mpira uliokuwa ukimilikiwa na mchezaji wa Werder Bremen
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni