Chama tawala nchini Zimbabwe
kimetuhumiwa kwa kuwanyima kwa makusudi msaada wa chakula wananchi
wanaounga mkono upinzani katika maeneo yenye baa la njaa kutokana na
ukame nchini humo.
Tume ya Haki za Binadamu ya Taifa
hilo imesema wapinzani wameambiwa na chama cha rais Robert Mugabe cha
Zanu-PF kwamba hawatopatiwa chakula cha msaada.
Rais Mugabe alitangaza hali ya
tahadhari mwezi Februari, huku serikali ikikadiria watu milioni nne
watahitaji msaada wa chakula ifikapo Januari 2017.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni