Mesut Ozil amefunga goli zuri la
dakika za mwisho lililoisaidia Arsenal iliyotoka nyuma kufungwa
magoli 2-0 na kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Ludogorets
Razgrad na kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ozil alilifunga goli hilo akiwa
ametulia baada ya kuudokoa mpira uliomshinda kipa na kukatiza
katikati ya mabeki wawili kabla ya kuutumbukiza mpira kimiani akiwa
karibu na goli la Ludogorets Razgrad.
Arsenal ambao walitaka kurudia kutoa
kipigo chao cha magoli 6-0, walijikuta wakikabiliana na upinzani kwa
kufungwa magoli mawili na Jonathan Cafu na Claudiu Keseru. Granit
Xhaka alifunga goli la kwanza kwa Arsenal na Olivier Giroud akaongeza
la pili.
Jonathan Cafu akishangilia kwa kukimbia baada ya kufunga goli la kwanza
Olivier Giroud akifunga goli kwa mpira wa kichwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni